L-ness alias LIONESS aka Lydia Owano Akwabi is one of East Africa’s top female Emcees. She has performed alongside other artistes at Hip Hop Halisi, Jukwaani, WAPI, Translating Hip Hop, Afreekah Album launch, Art & Beer Peace Festival, Alfajiri Album launch and the African Hip Hop Caravan shows. She released the albums Simangwe (2011), Gal Power (2012) and Punch (2013). Gal Power, launched at the Goethe Institute Nairobi in July 2012, exclusively features female Emcees from the East African region adressing empowerment of girls and women. L-ness facilitates workshops on hip hop culture, roots and traditions. In cooperation with Elimu Sanifu, an NGO supporting underpriviledged students, she has organized workshops in Starehe Boys Center and Girls High School (Nairobi). She completed a documentary on the growth and development of hip hop in Nairobi alongside TUMI, a South African MC from Johannesburg.

MATIBABU

Tiba ni kugawa visawa, dawa ni katiba ina usawa
Yawachunjuna yawakunakuna ka kichwani wana chawa
Maswala ya arthi, kanisa na koti za khadhi
Wepesi ndo uzito wa mama uaavyaaji
Usawa wa mali ugavi, umatajwa ukeeketaji, maji, ushuru kwa arthi?
Mjumbe? linani fulani halifiki mashinani kutilia maanani matakwa ya mwanamke mjini na mashambani
That’s why bado tuna haja ya haki ya usawa wa hali
See we’ve grown from little acorns now we’re mighty oak trees
Hekima twasimamisha ki mbuyu wa miaka alfu lela u lela ama mlima Kirimaara
Hadi mwenye shibe amtambue aliye na njaa
Bonge la gap vidonge na crap, meza zako tema zao
Wakauke ndimi tukija sisi kwa sisi kiCecily Mbarire
Vitenzi vyaja kiGrace Ogot
Mapambano naendeleza vile Winnie Mandela
Uliza wakamba wawili , nimesurvive kila vita
Iron fisted kiKarua
Motherly like Charity
Machungwa yaliyoiva kiJulia Ojiambo
Tupo halisi kiWangari Maathai kupigania miti
Mwangaza twasambaza kiEster Passaris
Hatutoki hatuchoki tuite maNdung’u Njoki
Uongozi mikononi kiSarah Godana na Agnes Ndetei
Saa hii si ndio rais wa watu
Ni rahisi kukukwuachu
Vichaa ka sisi tumekita mizizi vile vichaka sisi.

UPENDO KWOTE

Mimi namwomba Jire agape one love ya Rabbii
Mafarisayo masadusayo
wamefariiso kitako bila ngao
Love ni kuserve wanacounty inavyofaa
Wathii ka waturu waache kustarve
Uongezefu ushuru,
uhuru makanisani
madhabahu utakatifu upungufu
uongezefu uhalifu
bila upendo machiziwapo hali hafifu
onyesha upendo!
kama taabibu wa kweli, msaliti mbariki
sa imebaki wananchi kukaza mishipi
kwani upendo si kuvua skirt na chupi
bali ni kujikinga dhidi ya madhara ya whore of babylon
kwa kumulika na burning bush
burning good kush not gush
hii rhythm na harmony ziguse yako soul
tumake money tumake love not war

WAHENGA

Heri jua heri mvua
Si kiangazi si mafuriko
Si mimi ni mimi ni yeye
Ana kuni utosini na dogo mgongoni
Si mimi moyoni hadi bongoni mawazo fyongo
Ni yeye ametoka mtoni kuzoa waba
Mkononi vya sokoni, kuandaliwa makoni
Si mimi simtambui kiongozi tapeli wa kabila fulani

Ni yeye anapeperusha bendera hewani
Ni yeye anainua kazi ya watungaji
Ni yeye anataka amani irudi mitaani
Anapinga ufisadi anataka wathii wapate uradi
Police! Si mimi sijapata kuona upendo wa silaha na fimbo

Coz ni yeye ana kura ya kudai freedom
kutoka kwa ma slaves wa corruption
si mimi siko at ease ni yeye yuko attention
kuna waas in the hood!
kuna beef na hizi billz!
beef na bei ya bidhaa!
beef na bei ya ngataa !
beef na bei ya ungaa !
beef na gap ya rich na poor!